‘Dawa hizi zinatolewa bure’

Watanzania milioni 32.7 wachanja Covid-19

SERIKALI imesema dawa myeyuko za Amoxicillin, Zinki na ORS kwa ajili ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano zinatolewa bure na ni marufuku kuuzwa.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo leo Mei 12,2023 bungeni mjini Dodoma.

Amesema dawa hizo zinanunuliwa na serikali kwa kushirikiana na wadau na kusisitiza kuwa dawa hizo haziuzwi zinatolewa bure kwa wananchi.

Advertisement

Amesema katika kipindi cha Julai 2022 hadi Machi 2023, Wizara ilinunua na kusambaza dawa kwa ajili ya kutibu ugonjwa wa homa ya mapafu (Nimonia) ya kidonge myeyuko cha Amoxicillin vidonge milioni 30.1, na dozi 94,300 za Zinki na ORS kwa ajili ya matibabu ya kuharisha.

“Naomba kutumia fursa hii kusisitiza kwamba dawa za kidonge myeyuko cha Amoxicillin, Zinki na ORS kwa ajili ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano, zinanunuliwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau na dawa hizi hazipaswi kuuzwa,” amesema.

Amewaelekeza  waganga wakuu wa mikoa na halmashauri wasimamie suala hilo kwa ukamilifu.

Amesema ununuzi wa dawa hizo uliwezesha kuimarika kwa upatikanaji wa dawa za watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika vituo vya kutolea huduma kwa asilimia 90, ikilinganishwa na asilimia 85.3 katika kipindi hicho mwaka 2022.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *