Dawasa yapewa heko maendeleo ya miradi

DAR ES SALAAM; KAMATI ya Kudumu ya Bunge Uwekezaji na Mitaji ya Umma imeridhishwa na mwenendo wa miradi mbalimbali ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ikiwemo kuanzishwa kwa mradi wa maji taka ambao unagharimu zaidi ya Sh bilioni 128 ambao utakuja kuwa chanzo cha umeme.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Deo Sangu akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea utekelezaji wa miradi ya maji jijini Dar es Salaam amesema maendeleo ya mradi huo yanaridhisha na imani yao ni kwamba mradi huo utakwenda kurahisisha upatikanaji wa huduma za umeme.

Aidha, Sangu amesema kamati itaendelea kuwapa ushirikano Dawasa ili maji yasiwe kikwazo kwenye uzalishaji wa viwanda katika kuchochea pato la taifa na ajira kwa ujumla.

Advertisement

Kamati ya Bunge inaendelea na ziara katika miradi mbalimbali na kukagua maendeleo yake.

4 comments

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *