Dawasa yatoa ratiba mgao wa maji

MAMLAKA  ya Maji na Usafi wa Mazingira (DAWASA), imetangaza mgao wa maji kwa wakazi wa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Katika taarifa ya Dawasa, ratiba hiyo imeanza leo rasmi na maeneo ambayo yameguswa na mgao huo ni yale yanaoyohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu na Ruvu chini.

Kwa mujibu wa Dawasa, kila eneo litakuwa na mgao kwa siku mbili na ratiba hiyo ni ya wiki moja kuanzia leo Oktoba 27, 2022.

“Ratiba hizi zitatolewa kila wiki kwa kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa yatakayosababisha kuongezeka ama kupungua kwa maji katika mto Ruvu,” imesema taarifa hiyo ya Dawasa.

Kwa upande wa Ruvu chini, maeneo yanayokosa maji ni Boko, Tegeta, Kunduchi, Salasala, Mbezi Beach, Unioni, Wazo, Bagamoyo Mjini, Sunguvuni, Zinga, Viwandani, Kiharaka, Kerege na Mapinga.

Maeneo mengine ni Mikocheni, Kawe, Mbezi Juu, Goba, Kijitonyama, Mabwepande, Bunju Mkoani, Bunju B na A, Malolo, Mabwepande, Kinondo, Kibesa Teta, Mpiji Maputo, JKT, Mbweni Masaiti Bunju Beach, Mivumoni, Kilimahewa na Kinzudi.

Ratiba hiyo ya Dawasa inaonesha kuwa kesho Ijumaa maeneo yatakayokosa maji ni Mwenge,  Kijitonyama, Mwananyamala, Makumbusho, Kinondoni, Masaki, Mikocheni, City Center, Kariakoo, Mlalakua, Mlimani City, Chuo Kikuu, Keko , Temeke, Kigamboni, Magomeni, Tandale, Kigogo, Kilongawima, Kunduchi, Meko, Mtongani, Kisanga A & B na Mbezi Beach A na B.

Kwa upande wa maeneo yanayohudumiwa na Ruvu Juu leo Alhamis maeneo yanayokosa maji ni Unyamwezini, Tabata/Segerea, Kilungule, Kisukuru, Kwa Mkua, Kibangu, Makosa, Gide, Bucha, Baruti, Korogwe, Vinane, Tabata Msimbazi,Butiama, Kipawa, Stakishari viwandani (Nyerere Road),Kinyerezi Mbuyuni, Kinyerezi Kanga, Buguruni Madenge, Mwananchi, Tazara na Tabata Matumbi.

Maeneo mengine ni Tabata Relini, Tabata Shule, Tataba Barakuda, Tabata Bima, Aroma, Kibangu, Kajima, Novo, Liwiti, Maruzuku, Nyamani na  Ubaya Ubaya, Bonyokwa, Makongo, Kibamba, Temboni, Saranga, Malamba Mawili, Msuguri, Msingwa na Kimara B.

Maeneo yatakayokosa maji kesho Ijumaa ni Ubungo, Sinza, Magomeni, Mabibo, Manzese Mlimani City, Tandale, Mburahati, Takukuru, Lapaz, Rising Star, Damp, Brazil, Kanisa la KKKT, Royal Hostel, Kwa mama Mary, Kwa Fabiani, Hekima, Machimbo, Uzaramuni, Ngorongoro na Kwa mwanajeshi,

Mgao huo umeanza rasmi baada ya kupungua kwa vyanzo vya maji katika Mto Ruvu Juu na Ruvu Chini kutokana na kiangazi.

Habari Zifananazo

Back to top button