DC apokea wanafunzi Ubungo

MKUU wa Wilaya ya Ubungo mkoani Dar es Salaam, Hashim Komba amefanya ziara ya kuwapokea wanafunzi wa shule ya awali, msingi na sekondari ambao wameripoti kwa mara ya kwanza, baada ya ujenzi wa shule kukamilika.

Komba aliwapokea wanafunzi hao katika Shule ya Sekondari ya wasichana Dar es Salaam iliyoko Kwembe, ambayo ni miongoni mwa shule 10 maalum za sayansi zilizojengwa katika mikoa 10 nchini.

Pia aliwapokea wanafunzi wa shule ya awali na msingi katika Shule ya Goba Mpakani, ambayo ni mpya.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Dar es Salaam, Elizabeth Bonzo alisema mpaka leo tayari wamepokea wanafunzi 103, kati ya 215 waliotarajiwa.

Naye Mwalimu Mkuu wa Goba Mpakani, Luchana Mhapa amesema mpaka siku ya leo wamewapokea wanafunzi 802, kati ya hao wavulana ni 421 na wasichana 381.

Amesema shule hiyo ni mpya imechukuwa wanafunzi hao kutoka Shule ya Tegeta A, baada ya shule hiyo kuelemewa.

Amesema katika shule hiyo mpya wanafunzi wa darasa la awali waliopokelewa ni 120 kati ya 146 waliotarajiwa, pia wanafunzi wa darasa la kwanza walioripoti ni 162 kati ya 239 waliotarajiwa.

Habari Zifananazo

Back to top button