DC Arumeru: Elimu itolewe dhidi ukatili

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Emmanuela Kaganda ametoa rai kwa viongozi wa mila jamii ya wamasai (Malaigwanan)kukemea matukio ya ukatili yanayoibuka hivi sasa ikiwemo kutoa elimu sahihi juu ya matumizi ya teknolojia ya mawasiliano haswa simu za viganjani

DC,Kaganda ametoa ombi hilo Jijini Arusha wakati alipokutana na viongozi wa mila eneo la Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) ambalo ni eneo maalum la kufanyia mikutano yao ya jamii ya wamasai pia hulitumia kwaajili ya kufanya mambo ya mila ikiwemo kupata baraka.

Amesema endapo viongozi wa mila watatoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake,watoto na makundi mengine matukio ya ukatili yataweza kupungua sababu jamii itakuwa imepata elimu ya kutosh dhidi ya madhara yanayotokana na ukatili.

“Sijisikii vizuri kusikia matukio mbalimbali ya ukatili yanatokea katika wilaya yangu,naomba viongozi wa mila tushirikiane katika hili,lakini pia nawapongeza kwani kabila la wamasai ukweli ni kabila lenye kudumisha mila,tamaduni hivyo tushirikiane katika kuhakikisha utandawazi kupitia teknolojia ya simu za viganjani uwasaidie vijana kupata maendeleo badala ya kutumika kinyume na Tehama”

Pia DC,ametoa zawadi ya viti zaidi ya 20 zitakavyowawezesha viongozi hao kukaa wakati wanapofanya mikutano yao pamoja na mablangeti kwaajili ya baadhi ya viongozi hao kwaaili kujifunika na baridi.

Naye Katibu wa Malaigwanani hao,Amani Lukumay ameshukuru DC kufika eneo hilo muhimu kwaajili ya kujadili changamoto zao na kusisitiza kutoa elimu juu ya kupinga ukatili wa kijinsia,ndoa za utotoni na aina nyingine za ukatili kwa makundi mbalimbali ikiwemo utandawazi unaoharibu maadili kwa jamii hivyo endapo viongozi wa mila wakishirikiana na viongozi wa serikali na jamii mbalimbali

Awali mmoja kati ya waandaaji wa tamasha la Maasai Festival,Lekoko Lepilal amesema ujio wa Dc,Kaganda umeweza kuleta fursa lukuki kati ya serikali na viongozi hao wa mila kwani Agosti mwaka huu kutafanyika tamasha la kitamaduni litakalojulikana kama “Maasai Festival” litakalofanyika Mkoani Arusha .

Habari Zifananazo

Back to top button