DC ataka suluhu changamoto za wakulima wa Tumbaku

Onesmo Buswelu

MKUU wa Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi Onesmo Buswelu amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya hiyo kuhakikisha anakaa karibu na wakulima kupitia vyama vya ushirika (AMCOS) pamoja na Afisa ushirika ili kujua changamoto zinazo wakabili wakulima.

Ametoa maagizo hayo katika Mkutano Mkuu wa wakulima wa Tumbaku uliofanyika Kijiji cha Ifukutwa Kata ya Mpanda Ndogo wilayani humo,baada ya wakulima kuwasilisha malalamiko yao kuwa wapo baadhi ya mawakala ambao wanakataa kuwauzia mbolea aina ya NPK.

“Msamahazaji wa mbolea ambaye anafahamu utaratibu halafu anakataa kuuza NPK, kwa hakika serikali itachukua hatua kali kwake”amesema na kuongeza

Advertisement

“Taarifa ikitufikia usiku tunafanya kazi usiku huo huo,zikifika asubuhi tunafanya kazi asubuhi hiyo hiyo, hatuchelewi kwenye suala la kilimo kwa sababu kilimo ndiyo uchumi wa nchi yetu”

Hatua hiyo imemlazimu kutoa mawasiliano yake ya simu ya mkononi kwa wakulima hao ili waweze kumfikishia malalamiko yao moja kwa moja kuhusu changamoto wanazokumbana nazo za upatikanaji wa mbolea.

Hata hivyo,aliwataka wakulima wapatao elfu sitini walio salia kujiandikisha kwenye mfumo wa upataji mbolea ya ruzuku kujitokeza ili waweze kupata mbolea hiyo badala ya kulalamika.

Kwa upamde wake Mrajisi Msaidizi wa vyama vya msingi Mkoa wa Katavi Peter Nyakunga aliwaonya wanachama au viongozi wa vyama vya msingi wanao vuruga vyama lengo vivunjike na kisha waanzishe vyama vyao kwa tamaa za madaraka.

Awali, baadhi ya wakulima walilalamika kutofikiwa na pembejeo maeneo ya vijijini huku akihoji uwepo wa mbolea ya NPK kwenye ruzuku.