DC Bukombe aipongeza kampuni ya madini

MKUU wa Wilaya ya Bukombe, Said Nkumba ameipongeza kampuni ya madini ya ESAP kwa kutoa msaada wa vifaa vya elimu na afya wilayani humo kama sehemu ya kuunga mkono juhudi ya serikali katika kuboresha elimu pamoja na huduma za afya nchini.

Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo,  Said Nkumba amesema ESAP imekuwa mfano wa kuigwa kama kampuni ya wazawa zenye dhamira ya kuboresha huduma za kijamii kwa jamii zinazowazunguka.
“ESAP mmekuwa mfano wa kuigwa katika kampuni chache za wazawa zenye dhamira ya dhati ya kutekeleza dhana ya kurudisha kwa jamii. Nawapongeza kwa dhati kwa jambo hili kubwa mlilofanya katika kata hii ya Bulungwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Madini ya ESAP, Injinia Yahya Puyaga amesema zaidi ya Sh milioni 10 zimetumika kutoa msaada wa vifaa vya elimu pamoja na huduma vya afya wilayani humo.

“Sisi kama ESAP tunatambua juhudi za serikali ya awamu ya 6 katika kuboresha hudma za elimu na afya nchini. Hivyo leo tupo hapa Bulangwa kutoa msaada wa vifaa vyenye jumla ya thamani ya milioni 15, ikiwa vifaa elimu katika shule ya msingi Bulangwa vyenye thamani ya milioni 9 na vifaa tiba katika Zahanati ya Bulangwa vyenye thamani ya Sh milioni 6”.


“Esap Mining Services tumekabidhi madawati 50, vifaa vya michezo shuleni kwa wasichana na wavulana, vilevile uwekaji wa mfumo wa umeme katika nyumba ya walimu ambapo kwa pamoja gharama yake ni jumla ya Sh za Kitanzania milioni 9”

“Vile vile tumetoa msaada wa vifaa tiba katika Zahanati ya Bulangwa. Vifaa hivyo ni ni pamoja na kitanda cha uchunguzi kwa wagonjwa, Drip Stands, vifaa vya uchunguzi magonjwa yasioambukizwa kama kisukari na presha, vifaa vya kusafishia vifaa tiba vilivyitumika, pamoja na vifaa vya usafi,ambao kwa pamoja vifaa tiba hiyo vinajumla ya Sh milioni 6”.

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Julia
Julia
1 month ago

Every month start earning more than $12,000 by doing very simple Online job from home. I m doing this job in my part time i have earned and received $12,429 last month. I am now a good Online earner and earns enough cash for my needs. Every person can get this Online job pop over here this site.
.
.
Detail Here—————————————————————>>> http://Www.BizWork1.Com

Back to top button
1
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x