DC Ilala ataka viongozi wasiwe vikwazo

DC Ilala ataka viongozi wasiwe vikwazo

MKUU wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Edward Mpogolo amewataka viongozi kutokuwa vikwazo kwa mipango ya serikali inayopangwa ama kutatua shida za wananchi.

Mpogolo amebainisha hayo alipokutana na watendaji wa Tarafa ya Ilala wakiwemo viongozi wa kata, chama na serikali, wenyeviti wa serikali za mtaa, watendaji pamoja na viongozi wa matawi.

Katika kikao hicho, Mpogolo amewaambia watendaji hao ili wawe viongozi wazuri inabidi wawatumikie watu, kwani katika utumishi wa watu wanakuwa wanaimarisha chama, wanaimarisha serikali pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kupewa jina zuri na bora na wananchi anaowaongoza.

Advertisement

” Viongozi tushikamane, ushirikiano wetu na umoja wetu ndio ngao yetu,” amesema.

 

Pia amewataka watendaji hao kuutumia vizuri mfumo wa serikali za mtaa, aliohoji  kwa nini kuna tofauti kati ya viongozi wa chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali ilhali ni kitu kimoja?

Almesema ifike mahali mtu anapotaka kupima nguvu ya Ilala asipime kwa mtu mmoja mmoja bali kwa umoja wao bila kusema yule ni wa serikali na mwingine wa chama.

” Wapo wenyeviti wa mitaa wanaita mkutano kwa ajili ya wananchi viongozi wa matawi hawaendi,” amesema.

Almesema maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa  mwakani yanapaswa kuanza sasa hivi pasipokuwa na maelewano baina ya viongozi jambo hilo litakuwa gumu.

Amesema kwa upande wake ana wajibu kuwasemea vizuri wenyeviti wa serikali ya mtaa, madiwani, wabunge na Rais kwa mazuri yote wanayoyafanya.

” Niko tayari kutoa ushirikiano kwa kiongozi yoyote wa chama na serikali,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Majengo, Kata ya Vingunguti, Chande Msoke amemshuru mķuu huyo wa  wilaya kwa kuamsha watendaji na wenyeviti wa serikali za mtaa kwamba kila mmoja anapaswa kutambua wajibu alionao.

Amesema kuna wakati ulifika viongozi wa serikali kulipofanyika mikutano ya chama walijiona wao kama sio sehemu ya mkutano huo.

/* */