DC Ilala: Zuieni rushwa

MKUU wa Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, Edward Mpogolo ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kujikita zaidi katika kuzuia Rushwa badala ya kupambana nayo.

Akizungumza jana katika hafla ya ufunguzi bonanza la wapinga rushwa 2024 linalofanyika katika viwanja vya Jakaya Kikwete (JMK Park), Mpogolo amesema kusubiri rushwa itokee ili upambane nayo ni kuchelewesha haki.

“Lakini jambo kubwa mnalofanya ni kupambana na rushwa. Ukisubiri ukapambane na rushwa tayari mtu ameshaumia, kama ni mtoto amekwenda kufanya mitihani, mitihani yake imefutwa. Na kama unampeleka mahakamani mla rushwa unaendelea unaendelea kutumia gharama”. amesema

Mpogolo ameipongeza TAKUKURU Mkoa wa Ilala kwa kuwa mstari wa mbele kutoa elimu ya rushwa. Amesema kutoa elimu ya rushwa kwa vijana hao ni kuunga mkono kwa vitendo jitihada za Rais Samia.

“Nimepita mikoa mingi, ni mikoa michache ambayo makamanda wa TAKUKURU wanaandaa shughuli kubwa za elimu kama shughuli hii ya leo, hivyo kama ndugu yangu na rafiki yangu naomba nikupongeze wewe pamoja na timu yako. Mmekuwa vinara wa kuonesha ni namna gani tunamuunga mkono mh Rais kwa kutoa elimu kuhusu tatizo la rushwa”.  Aliongeza

Habari Zifananazo

Back to top button