DC Karatu aitaka Tarura kutatua shida miundombinu

MKUU wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha ,Dadi Kolimba amewataka watumishi wa Wakala wa Barabara Vijijini (TARURA) Mkoa wa Arusha kutatua changamoto za miundombinu kabla ya kuanza mvua za El-Nino zilizotangazwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa.

Kolimba ameyasema hayo wakati akifungua kikao Kazi cha watumishi wa Tarura kinachofanyika kwa siku mbili wilayani Karatu ambapo amesema taarifa za mamlaka ya hali ya hewa nchini kuwepo kwa mvua hizo ni vyema kujipanga sawia kutatua changamoto za miumdo mbunu kwa wananchi kabla na baada ya mvua hizo.

“Kuna shughuli ambazo zinatakiwa kufanyika kabla ya maafa lakini kunashughuli zinatakiwa kufanyika wakati wa maafa na Kuna shughuli ambazo zinatakiwa kufanyika baada ya maafa na sekta yenu ni muhimu sana Sasa tukahakikishe katika ile mipango yetu tunaisimamia vizuri ilimvua hizi zinapo nyesha zisilete maafa makubwa kwa wananchi kama kama alivyo elekeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan”. Amesema Kolimba.

“Maeneo yote ambayo yamekuwa na changamoto mkayaweke vizuri kwa kuzibua mitaro kuweka makaravati kabla ya athari Kubwa haijatokea kwa kuhakikisha tunaisimamia vizuri ili mvua zinapokuja tusiwe na madhara makubwa na hasa mkafanye kazi za kitaalam zaidi na kushirikia na wananchi maana wao ndiyo wanajua maeneo yenye madhara makubwa kioindi cha mvua”. Aliongeza Kolimba.

Aidha aliwataka madiwani kutoweweseka kwa kila mmoja kuvutia kwakwe na badala yake washirikiane na wataalam wa Tarura ambao wamepewa dhamana ya kufanya kazi hiyo ambayo ni muhimu sana kwa ustawi wa Taifa letu hasa katika ukuaji wa uchumi unatengemea miundombinu iliyo bora.

“Sisi sote tunalo jukumu Kubwa la kuhakikisha barabara zote za vijijini na mijini zimekaa vizuri ili kusaidia kusitokee maafa makubwa na kukuza uchumi wetu maana biashara zetu zinatengemea hasa miundo mbinu, kupitia kamati za wataalamu kuanzia ngazi za kata wilaya hadi Mkoa tujiandae ipasavyo endapo yatatokea maafa tuhakikishe tunatumia vizuri Elimu zetu kuokoa ili kusitokee madhara makubwa”. Alisema Kolimba.

“Wakati Mimi naingia hapa Karatu mwaka 2021 tulipata bajeti ya Sh million 928 lakini kwa mwaka wa fedha 2022/23 tumeanza kupata bajeti ya Sh billion 2.3 ambapo Wilaya ya Karatu Ina mtandao wa barabara kilometa 712 wakati naingia tulikuwa na barabara za lami km 0.6 Sasa tuna km 2.8. haya ni maendeleo makubwa yanayo fanya na kutekelezwa na Rais wetu Samia Suluhu Hassan katika kuchechea uchumi wa wana Karatu”. Aliongeza Kolimba.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Tarura Mkoa wa Arusha Mhandisi Albart Kyando amesema kikao hicho ni maalumu kukujadili mambo mbali mbali ya kiutendaji hasa kuweka kuiweka miundombinu bora ya viwango na pia wamepokea maelekezo ya Mkuu wa Wilaya na wameshaanza kuchukuwa hatua za kujikinga kwa kuandaa Mpango mkakati kama taasisi wa kukabiliana na mvua hizo.

“Kwa Sasa tunakazi zilizofanyika tumepokea tahadhari tokea mwezi wa 7 na Kazi ya kwanza ilikuwa ni Madaraja na vivuko vyote pale penye changamoto tumeshaanza kuchukuwa hatua kwa kutenga baadhi ya rasilimali ambazo tulikuwa tutumie katika Kazi za kawaida tumeelekeza huko hivyo itakapotokea tutaendelea kukabiliana ili kupunguza athari”. Alisema Kyando.

“Mara nyingi bajeti zetu tumekuwa tunapanga kulingana na kufungua barabara mpya kutokana na vyanzo vya mfuko wa Jimbo na tozo kwa kipaumbele cha kwanza kuwa maeneo ya uzalishaji kwa kuongeza nguvu hivyo ni lazima tuwe na vipaumbele vya ujenzi ili kuondoa migogoro tumekuwa tukitoa Elimu kwa wananchi na madiwani “. Aliongeza Kyando

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button