DC Kigamboni atoa neno malezi ya watoto

MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo amewataka wazazi kusimamia maadili ya watoto wao dhidi ya mmomonyoko wa maadili pamoja na kukemea biashara za ngono zinazofanywa ndani ya vilabu vya pombe za kienyeji maarufu ‘ubanda’.

Kauli hiyo ameitoa leo Juni 07, 2023 wakati wa kusikiliza na kutatua kero za wananchi wa kata ya Pembamnazi wakitaja ubovu wa barabara, ukosefu wa maji ya uhakika, migogoro ya ardhi, kutokuwa na usafiri wa uhakika.

Advertisement

Bulembo amekagua miradi ya maendeleo ikiwa ni muendelezo wa ziara yake iliyoanzia kata ya Pembamnazi yenye mitaa 15, lengo likiwa ni kujitambulisha na kueleza mikakati yake katika kuwatumikia wananchi.

“Awamu ya kwanza tumefanya vikao na wananchi kuhusu ubanda, awamu ya pili ni kubandika ‘notice’ za katazo na baada ya hapo tukikukuta, tutawakamata.”

DC Bulembo amekemea uvunaji wa mikoko kiholela akisema kuwa hilo ni kosa kisheria na kwani huharibu mazingira lakini pia huzorotesha juhudi za serikali kugharamia uoto huo.

“Wilaya ya Kigamboni ndio eneo pekee lililobaki upepo unapovuma maeneo mengine wanategemea Kigamboni kuja kupunga upepo kwahiyo inapotokea uharibifu wa mazingira, mnataka waende wapi Zanzibar.?”

Kwa upande mwingine Bulembo amekemea uvuvi haramu kwakuwa ni uchafuzi wa mazingira na uharibifu wa mazalia ya samaki na viumbe bahari

Aidha, ametaka kusitishwa mara moja kwa biashara za magendo kwa kusema huo ni uhujumu uchumi kwani wanaikosesha mapato serikali.

“Tupo katika oparesheni maalumu kwa wote wanaopitisha na kusafirisha biashara za magendo na tukiwakamata utashitakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi.”

Hata hivyo, mkuu wa Wilaya amesema serikali imetenga bilioni 1.9 kwajili ya ujenzi madarasa ya shule nne wilayani humo sambamba na bilioni 1.5 kwaajili ya kuongezea nguvu miradi ya mbalimbali ya maendeleo ya wilaya ikiwemo soko la kimkakati Kibada,  ujenzi wa barabara na zahanati katika kila kata.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *