DC Korogwe aiomba Tamisemi kuingilia kati suala la wakurugenzi

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Basila Mwanukuzi amemuomba Waziri wa Tamisemi, Angela Kairuki kuingilia kati hujuma inayofanywa na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya hiyo kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu ikiwemo kusimamia miradi ya maendeleo .

Mkuu wa wilaya huyo ametoa ombi hilo leo wakati akiongea na waandishi wa habari kutokana na kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye wilaya hiyo.

amesema kuwa miradi mingi ya maendeleo katika wilayaimekuwa ikisuasua kutokana na wakurugenzi kushindwa kutekeleza majukumu hali ambayo inasababisha baadhi ya fedha za miradi kurudishwa serikali.

“Tupo hapa kwaajili ya kumsaidia Rais Samia lakini wengine wapo kwaajili ya kunikwamisha na kunigombanisha Rais na wananchi sitokubali jambo hilo na namuomba sana waziri wa Tamisemi aingilie kati swala hili kwani ni hujuma “amesema DC huyo

Habari Zifananazo

Subscribe
Notify of
guest
0 Comments
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button
0
Would love your thoughts, please comment.x
()
x