DC Kwimba awafariji familia ya mtoto aliyeliwa na fisi

Mkuu wa Wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza, Johari Mussa Samizi, ametoa pole kwa familia ya mtoto Emanuel Marco Nyagela, mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa Kijiji cha Mwangika, Kata ya Mwabomba aliyefariki baada ya kuliwa na fisi wakati akienda kuoga kwenye dimbwi na wenzake.

Akizungumza na familia ya mtoto huyo leo Desemba 29,2022, Johari Samizi amesema akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, ameunda kikosi maalum kuwasaka fisi.

Ametoa pole na kuwaasa wazazi na walezi kuwa na uangalifu katika kuwalinda watoto wadogo.

Emmanuel Nyagela (3) alifariki dunia Desemba 27,2022 saa 12 jioni kijijini hapo, baada ya kunyakuliwa na fisi na kutokomea naye msituni, wakati akienda kuogelea kwenye dimbwi na wenzake, ambapo baba wa mtoto huyo aitwaye Marco Nyangela, alisema alisikia yowe kutoka kwa wanakijiji wakisema mtoto wake ameliwa na fisi, ndipo wakaanza kumsaka mtoto huyo na kuishia kuona damu zikiwa zimetapakaa kuelekea kwenye msitu huo.

Taarifa zinaeleza kuwa hadi kufikia Desemba 28, 2022 asubuhi wamefanikiwa kuona nguo alizokuwa amevaa mtoto huyo na baadhi ya viungo vya mwili wake.

Habari Zifananazo

1 Comment
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button