DC Lushoto ataka mikakati mazao ya biashara

TANGA: MKUU wa Wilaya ya Lushoto, mkoani Tanga Japhari Kubecha amewaelekeza maofisa kilimo wa wilaya hiyo kuandaa mpango mkakati wa kilimo kwa miaka mitano ambao utaonesha kila kata kuwa na zao la kimkakati la biashara.

Akizungumza katika kikao na wadau wa kilimo, umwagiliaji na maofisa ugani wa wilaya hiyo, Kubecha amewataka pia maofisa kilimo kwenye maeneo kuwasikiliza na kutatua changamoto za wakulima.

“Ipo mikakati ya kitaifa, lakini tukasema na sisi tuandae mikakati ya wilaya, naamini sio kila mahali panakuba kila zao, naamini iko kata fulani zao fulani litakuwa linakubali, muhimu tuweke mikakati hapa namna gani kata hiyo tunaenda kuweka msukumo kwenye zao fulani.

Advertisement

Pia Kubecha amewataka maofisa umwagiliaji wa wilaya hiyo kufanya utafiti wa kina wa kubaini maeneo yanayotakiwa kuongezwa tija kwenye umwagiliaji.

“Mliacha maeneo ya mifereji, muende mkafanye tathmini tuandike andiko nilishatoa maelekezo kupeleka kwenye tume ya umwagiliaji tuone namna gani mifereji tunaisadia kuwekewa bajeti na kufanyiwa upembuzi na ukarabati,” amesema DC Kubecha.