DC Mbogwe atoa elimu ya lishe

GEITA: Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita, Sakina Mohamed ametoa elimu ya lishe kwa wananchi wa wilaya hiyo na kuwataka kubadili namna ya ulaji wa vyakula ili kuepukana na changamoto mbalimbali zinazotokana na ulaji mbaya.

Sakina ameshauri umuhimu wa kuzingatia lishe bora yenye makundi kamili na sio kushiba kama ilivyozoeleka kwa jamii nyingi ikiwepo wana Mbogwe.

Amesema. lishe bora husaidia mwili kukua vyema, kuujenga mwili lakini pia huimarisha kinga ya mwili ili kuweza kupigana na magonjwa.

“Ili lishe iwe bora ni muhimu iwe na mchanganyiko wa vyakula mbalimbali kama vile protini, wanga, fati, mbogamboga, madini, matunda na maji kwa wingi,”amesema.

Sakina ameyasema hayo leo Februari 14, 2024 katika kituo cha afya cha Masumbwe ambapo pia alishiriki zoezi la kupika uji na kunywa na watoto katika kituo hicho.

‘’Lishe bora inaanza na namna ya ulaji kwani lishe bora sio kula na kushiba hivyo watoto na vijana kama taifa la kesho tunapaswa kuzingatia namna ya ulaji bora kuepuka changamoto mbalimbali za kiafya ikiwemo ugonjwa ya moyo,”amesema Sakina

Aidha, Sakina amesema lishe ni mchakato unaohusisha hatua mbalimbali kuanzia chakula kinapoliwa, kumeng’enywa, na hatimaye virutubishi kufyonzwa na kutumika mwilini na atimaye kuleta afya, kimwili, kiakili na kisaikolojia.

Amesema makundi matano ya vyakula ikiwemo matunda, pia amepata fulsa ya kutoa limu ya malezi, makuzi, na maendeleo ya watoto kuanzia umri 0 hadi miaka nane.

Habari Zifananazo

Back to top button