DC Mkinga apewa maagizo wahamiaji haramu

TANGA; Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dk Batilda Burian amemuapisha Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Gilbert Kalima na kumuagiza kuweka mikakati ya kupambana na wahamiaji haramu, magendo pamoja rushwa.

Pia Dk Burian amemuagiza Mkuu huyo wa Wilaya kusimamia hali ya upatikanaji wa bidhaa muhimu kama vile sukari na mafuta na usimamizi wa bei zilizotolewa na serikali katika msimu huu wa mfungo wa Ramadhan.

Advertisement

“Najua uwezo wako kwani uliweza kuimarisha vema Jumuiya ya wazazi Taifa, hivyo ni Imani yangu hata Mkinga nako utaweza kufanya vizuri zaidi, kikubwa ni kuhakikisha tunainua kipato cha wananchi na kupambana na magendo na wahamiaji haramu,”amesema Mkuu wa mkoa .

Kwa upande wake Kalima baada ya kuapishwa alimshukuru Rais Dk Samia Suluhu Hassani kwa kuwa na imani ya kumchagua na kuahidi kusimamia yale yote ambayo Rais Dk Samia Suluhu Hassani, atamani yafanyike katika Wilaya ya Mkinga.

“Kikubwa niwaombe watumishi wenzangu ushirikiano wa kutosha hususani katika eneo la utekelezaji wa Ilani ya CCM kwa kuhakikisha tunatekeleza katika viwango bora,”amesema Kalima.