DC Mkinga kuchunguza miradi ya Sh milioni 737

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdurahman amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Maulid Surumbu kufanya uchunguzi wa matumizi ya fedha zaidi ya Sh milioni 737 zilizotumika katika ujenzi wa shule na zahanati wilayani humo.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ziara yake wilayani Mkinga ya kukagua miradi ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Kigongoi itakayogharimu Sh milioni 670 zahanati ya kijiji cha Nzigi Mwagogo uliyogharimu Sh milioni 67 .

Amesema kuwa kutokana na kutokamilika kwa miradi hiyo Kwa wakati na kusababisha kero Kwa Wananchi hivyo ni vema Mkuu wa Wilaya hiyo kufanya uchunguzi na iwapo kutabainika ubadhirifu hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa.

“Wananchi wanaendelea kuteseka kwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma ya afya na elimu kutokana na kutokumalizika kwa miradi hiyo ambayo dhahiri inaonekana imekosa msukumo wa watendaji katika swala zima la usimamizi”amesema Mwenyekiti Rajab

Nae Mbunge wa Wilaya ya Mkinga Dastan Kitandula amekiri ujenzi wa miradi hiyo mitatu imechukua muda mrefu kumalizika kutokana na changamoto ya kifedha na migogoro ya wananchi na kumuomba Mwenyekiti huyo aweke msukumo ili miradi hiyo iweze kukamilika na iweze kutumiwa na wananchi wa Kijiji hicho .

Habari Zifananazo

7 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button