MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Dustan Kyobya leo amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Meneja Huduma za Habari za Lugha za Kigeni, Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Christopher Majaliwa, kuhusu fursa za kimaendeleo zilizopo katika Wilaya na Mkoa wa Mtwara.
Viongozi hao pia walijadili mikakati ambayo itawezesha kutangaza fursa hizo za kimaendeleo, ikiwemo uwekezaji katika mkoa wa Mtwara kupitia magazeti ya TSN ambayo ni Daily News, HabariLEO, SpotiLeo na mitandao ya kijamii iliyo chini ya TSN, pamoja majarida maalumu ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za serikali