DC Tandahimba awapa neno wanahisa Tacoba

WANAHISA katika Benki ya Wananchi Tandahimba (TACOBA) mkoani Mtwara wametakiwa kuendelea kununua hisa ili kuongeza thamani ya uwekezaji wao.

Hayo yameelezwa wakati wa mkutano mkuu wa kumi wa wanahisa wa benki hiyo mwaka 2024.

Mkutano huo umefanyika jana Machi 19, 2024 wilayani Tandahimba mkoani Mtwara ukiambatana na mkutano mkuu wa kwanza wa wanachama wa Tandahimba Cooperative Benki Limited.

Advertisement

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Kanali Michael Mntenjele amesema wanahisa hao waendelee kupanua wigo wa benki hiyo ili wapate manufaa zaidi ikiwemo kuongeza mitaji kwenye hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Newala mkoani humo Rajabu Kundya amesema serikali inaunga mkono na kufurahia kujionea mafanikio wanayoyapa wanahisa katika benki hiyo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tacoba Mohamed Nassoro amesema kwa hesabu za mwaka 2023 benki hiyo ilikuwa na mtaji wa Sh bilioni 2.284.

Meneja Mkuu wa Tacoba Yahya Kiyabo amesema mwaka 2023 amana za wateja ziliongezeka kwa asilimia 49 hadi kufikia Sh bilioni 1.7 ikilinganishwa na amana za Sh bilioni 1.2 kwa mwaka 2022.

Mkuu wa Fedha na Uendeshaji wa Tacoba, Julius Sawaya amesema mapato ya jumla yaliongezeka kwa asilimia 0.2 na kufikia Sh milioni 729 mwaka 2023 kutoka Sh milioni 727 mwaka 2022.

Mwanachama wa benki hiyo, Ahmed Ahmed “Niwaombe wanahisa wenzangu tuendelee kuwekeza kwenye benki yetu ili tutengeneze mtaji mkubwa kwenye benki yetu”

Katika hatua nyingine wanachama hao wamepitisha azimio maalum la kuidhinisha kuunganisha vyama vya Tandahimba Cooperative Benki Limited na Kilimanjaro Cooperative Benki Limited.

Hilo limekuja kupitia muungano wa vyama vya ushirika ili kuanzisha kwa pomoja benki ya ushirika tanzania