MKUU wa Wilaya ya Ubungo Heri James amesema serikali inaendelea kuthamini mchango wa walimu na kuwajali, hali inayodhihirishwa na uwekezaji uliofanyika kwenye sekta hiyo ya elimu.
Mkuu huyo wa Wilaya aliyasema hayo wakati alipozindua kampeni ya ‘Asante Mwalimu’ yenye lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika kuhakikisha walimu wanakuwa na mazingira bora ya utoaji elimu.
Alisema katika maboresho hayo walimu wanalipwa malimbikizo na stahili zao, wanakwenda likizo kwa wakati na kupanda madaraja kwa wenye sifa na vigezo stahili.
“Mwalimu ni mtu muhimu hakuna namna tunaweza fanikiwa bila mwalimu,” alisema James.
Alisema kupitia kampeni hiyo pia imeambatana uzinduzi wa bando la mwalimu ambalo ni mkusanyiko wa bidhaa zinazomlenga mwalimu zikiwa na lengo la kumpatia suluhisho la kifedha zaidi.
Alisema pia bando mwalimu imelenga kumlinda mwalimu na athari kubwa za mikopo umiza ambayo ni kilio kikubwa cha walimu nchini.
“Hivyo utulivu wa mwalimu unabebwa na Mwalimu benki kwa kupata huduma bora za kibenki kwa gharama nafuu sana,” alisisitiza James
Aliipongeza Benki ya Mwalimu kwa kuijali sekta ya elimu na kuanzisha huduma hiyo ya bando la mwalimu itakayomsaidia mwalimu tangu akiwa chuo.
“Serikali inajivunia sana uwepo wa Mwalimu Benki,” alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo cha Biashara kutoka Benji ya Mwalimu Leticia Ndongole alisema kampeni hiyo imekuja wakati dunia ikielekea katika maadhimisho ya Siku ya Mwalimu Duniani.
“Kampeni hii imelenga kurudisha shukran zeti za dhati kwa walimu Kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kuelimisha na kukuzq Taifa kwa ujumla,” alisema Ndongole.
Alisema bando la Mwalimu no mkusanyiko wa bidhaa zinazoendana sambamba na safari ya maisha ya Mwalimu.
Alieleza kuwa benki hiyo inaanza na Mwalimu tangu akiwa mwanafunzi, anapoanza kazi, maisha yake ya ajira, anapojiandaa kustaafu na maisha baada ya kustaafu.
“Mwalimu ni wa kwetu hatumuachi hata hatua moja,,” alisisitiza.
Alitaja bidhaa zinazopatikana kwenye bando la Mwalimu kuwa ni akaunti maalumu Kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu na Mwalimu jikimu akaunti inayotoa mikopo maalumu kwa walimu wanapoanza ajira.
Bidhaa nyingine ni Ada chapchap, salary advance, mkopo wa dharura wenye kiwango kikubwa cha fedha na mkopo binafsi wa Mwalimu.
Pia, bando Mwalimu inatoa huduma ya mkopo maalumu wenye riba nafuu kwa wastaafu wanaosubiri kulipwa mafao ya kiinua mgongo na mkopo maalumu kwa wastaafu.