DCEA yatoa elimu matumizi dawa za kulevya

MAMLAKA ya Kudhibiti Dawa za Kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imetoa elimu kwa waraibu zaidi ya 150 wanaotumia dawa za hizo ili waache kutumia ikiwemo kutumia kliniki zilizopo nchini kwa ajili ya kupata huduma za matibabu na ushauri wa kuacha kutumia dawa hizo.

Mafunzo kwa waraibu hao wa Dawa za Kulevya yamefanyika Chuo Cha Ufundi Arusha (ATC) na kuandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya Kanda ya Kaskazini ambapo Shaban Miraji ambaye ni Ofisa Msimamizi wa Elimu kutoka Mamlaka hiyo Kanda ya Kaskazini alisisitiza umuhimu wa mafunzo hayo kwaajili ya kuacha matumizi hayo.

Elimu hiyo imekuja kwa warahibu hao kutokana na mikoa ya Kanda ya Kaskazini,Arusha, Kilimanjaro,Tanga na Manyara ndio inayoongoza kwa matumizi ya dawa za kulevya ikiwemo mirungi na aina nyingine za dawa za kulevya ikiwemo kufanya mambo yasiyofaa kwa jamii.

Amesema mafunzo hayo yanalengo la kudhibiti matumizi hayo kwani katika kipindi cha miezi mitatu Septemba hadi Desemba mwaka huu mamlaka hiyo imefanya oparesheni katika maeneo mbalimbali ya kanda hiyo na kukamata magunia ya bangi zaidi ya 237 na mbegu za bangi kilo 310 ,mirungi kilogramu 1.534 na heroin kadhaa ambapo Mkoa wa Kilimanjaro kwakushirikiana na vyombo vingine vya usalama walikamatwa gunia mbili za mirungi ,kilo moja ya banhi na heroin gramu 1 .5 ,Huku watuhumiwa 36 wakimatatwa na kesi 17 zilifunguliwa.

Pia elimu kwa umma iliweza kutolewa kwa watu zaidi ya 12,469 kutoka tàasisi 15 vikiwemo shule za msingi na sekondari, taasisi za serikali,vyuo,maeneo ya tiba zkata na mitaa mbalimbali wakiwemi waraibu kwaajili ya kuondokaba na matumizi hayo.

“Tumewaita katika tiba na mwamko ni mkubwa hivyo tunawaomba waachane na dawa hizi na tunatumia wasanii pia ili kufikia kundi kubwa la vijana na pia kuna wenye vipaji tutawaendeleza zaidi ili waachane na dawa hizi na dawa za kemilaki zinaharibu meno kuozesha na watumiaji wa mirungi wanaua ini”

Naye mmoja kati ya waraibu hao, Naomi Massawe amesema alianza kutumia dawa hizo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita alipokuwa alifanya kazi za uchimbaji madini Mirerani lakini sasa katika kipindi cha miaka miwili ameacha kutumia dawa hizo na sababu kubwa iliyopelekea kuacha dawa hizo ni mtoto wake kila akiona vituko vya mama yake huyo analia na sasa hivi anaendelea kupata mafunzo mbalimbali yaliyomsaidia kuachana na dawa hizo

Wakati huo huo,Dk, Said Salum ambaye ni Mkuu wa Idara ya Afya na Kitengo cha Dawa ya Methodone kutoka Hospitali ya Mount Meru, amesisitiza huduma za matibabu kwa warahibu hao zinatolewa bure hivyo wafike hospital zilizopo katika mikoa hiyo kupata matibabu hayo sanjari na matumizi sahihi ya uzazi wa mpango kwa wale wanaokuwa wajawazito.

Habari Zifananazo

Back to top button