‘Debora Mwenda ni namba nyingine’

DAR ES SALAAM: Bondia Debora Mwenda kutoka Fire Stone Gym ametamba kumtwanga mapema mpinzani wake Samira Kasimu kwenye pambano la ‘Hatukimbii Hatuogopi’ linalotarajiwa kufanyika Aprili 11, 2024.

Akizungumza wakati akiendelea na maandalizi yake akiwa Gym Temeke Dar es salaam Debora amesema Samira Kassim ajiandae kwani yeye ni namba nyingine.

“Samira atake asitake kipigo lazima hivyo ajiandae na kichapo cha paka mwizi kwenye pambano atajuta kuchagua kupambana staki mchezo.”amesema Debora Mwenda.

Katika siku ya pambano hilo bondia,Karim Mandonga atapanda ulingoni kuzichapa na Mada Maugo.

 

 

Habari Zifananazo

Back to top button