DECCA chini ya ulinzi

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (Nactvet) limekiweka katika uangalizi maalum katika kipindi cha miaka mitatu Chuo cha DECCA Afya na Sayansi Shirikishi (DECOHAS)- Dodoma kutokana na kukiuka taratibu za udahili.

Chuo hicho kimehusika na udahili wanafunzi 17 kwenye kozi ya afya ya jamii ambayo ilifutwa mwaka 2019.

Akizungumza leo Oktoba 5, 2023 jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa udhibiti ubora Nactivet Dk Jofrey Oleke amesema wanafunzi wote waliopitia mkasa huo tayari wamerudishiwa gharama zao zote na chuo kuwekwa kwenye uangalizi mkali.

Hatua hiyo ya Nactvet imekuja baada ya wanafunzi Wanafunzi 17 wanaodaiwa kusoma kozi ya Afya ya Jamii (Community Health) katika chuo hicho kutimuliwa na uongozi baada ya kugomea mtihani wa mwisho wa kozi hiyo kwa kile walichodai kuwa haitawasaidia kupata ajira kwani hawatambuliki kwa sababu hawajasajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (Nacte).

Habari Zifananazo

2 Comments
Oldest
Newest Most Voted
Inline Feedbacks
View all comments
Back to top button