Deo Champion ageukia injili

BINGWA wa muziki wa dansi nchini mwaka 1999/2000 Deus Boniface maarufu Deo Champion amesema ameamua kujikita katika uimbaji wa nyimbo za injili kutokana na kupitia magumu mengi katika maisha yake ya sanaa.

Deo aliyeshinda pia katika shindano la vipaji la Club Raha Leo amesema licha ya kuwa maarufu, fedha na vitu vingi lakini bado hatokuwa na furaha kama hatomsifu na kumuimbia Mungu wake.

“Nimeshinda mashindano mengi ndani na nje ya nchi, nimepata mafanikio makubwa zikiwemo fedha lakini bado sitakuwa na furaha kama nitaendelea kuimba nyimbo za kidunia naona bora nitimize shahuku yangu nikiwa hai kwa kumuimbia Mungu” amesema Deo

Deo aliyetamba na wimbo wa ‘Shemeji’ anasema amepitia mambo mengi magumu katika maisha yake ikiwemo kunyang’anywa mtoto wake lakini hakuteteleka sababu ya imani yake kwa Mungu.

“Nilipokonywa hadi mtoto wangu sababu sikuwa na uwezo kifedha nina huzuni sana naamini nikiimba kumsifu na kumshitakia Mungu, huzuni yangu itakwisha nitakuwa na furaha tena,” alisema Deo Championi ambaye kwa sasa anaendelea kucheza disko na kufanya mazingaombwe katika shughuki za harusi mbalimbali anazoharikwa.

Habari Zifananazo

Back to top button