Dera linamnogesha mwanamke

DAR ES SALAAM; Dera ni vazi la heshima kwa wanawake linalofanya mwili kuwa huru.

Vazi hili huvaliwa sehemu yoyote, humfanya mtu kuheshimika na kuonekana mstaarabu.
Zamani ilionekana kama vile dera au madera yakivaliwa na wanawake wa imani fulani tu.

Lakini siku hizi mambo yamebadilika na kila mwanamke anavaa na kuonekana kupendeza.

Advertisement

Yapo madera ya aina tofauti  kuna yakushonwa kwa kutumia kitambaa na yapo yanayotoka nchi za Falme za Kiarabu, India, Uingereza na Somalia.

Pia kuna madera ya kisomali yanayotokea Mombasa, Kenya. Haya yamepewa jina maarufu kama vijora. Ukienda katika baadhi ya harusi mitaani huko, vijora ndiyo sare maarufu ya harusi kwa wadada.

Dera huwa halimkatai mtu lakini pia ni vazi la heshima, ambalo mwanaume akiona mwanamke amevaa anatafsiri ni mwenye heshima na  anastahili kuwa mlezi wa familia.

Vazi hili halimkatai mtu si mnene wala mwembamba , mweusi au mweupe, mrefu ama mfupi akivaa anapendeza.