Philipo amesomewa shitaka hilo leo Novemba 10, 2023, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Amani Sumari, ambapo Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Monica Mweli amedai mshitakiwa alitenda kosa hilo Novemba Mosi, 2023 eneo la Nyamhongoro Wilaya ya Ilemela.
Mhina ambaye ni dereva wa gari ya Shule ya Msingi Nyamuge ya jijini Mwanza akiwa anarudisha nyuma gari hiyo yenye namba za usajili T.964 BRJ aina ya Mitsubishi Rosa, baada ya kukamatwa na kosa la usalama barabarani alimgonga Sajenti Stella na kusababisha kifo chake.
Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa amekana kosa na kurejeshewa rumande kutokana na kutokidhi vigezo vya dhamana, ambapo alitakiwa kuwa na wadhamini wawili na barua ya Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa kila mmoja. Kesi imeahirishwa hadi Novemba 23, 2023 itakapokuja tena kwa ajili ya mshitakiwa kusomewa maelezo ya awali ya shitaka linalomkabili.
Comments are closed.