Dereva mbaroni kwa kubaka, kutomasa watoto

JESHI la Polisi Mkoa wa Songwe limemkamata dereva wa bajaji katika mji wa Vwawa wilayani Mbozi, Ayubu Mng’osi (30) kwa tuhuma za kubaka na kufanya shambulio la aibu kwa watoto wawili wenye umri wa miaka 7 na 9 ambao ni wanafunzi wa shule ya  msingi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Theopista Mallya alisema katika tukio la kwanza, mtuhumiwa huyo anadaiwa kumwingilia kimwili mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya Msingi Ichenjezya (Jina limehifadhiwa).

“Mbinu aliyotumia mtuhumiwa ni kumlaghai mtoto na kuingia naye ndani ya nyumba anayoishi kisha kumwingilia kimwili” amesema.

Advertisement

Aidha Kamanda Theopista amesema kuwa mtuhumiwa huyo pia anadaiwa kumfanyia shambulio la aibu la kumshika na kumchezea sehemu za siri mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya Ichenjezya Wilayani Mbozi (naye jina limehifadhiwa).

“Julai 14 mwaka huu maeneo ya Mianzini Kata ya Ichenjezya mtoa taarifa aligundua kushikwa, kuchezewa sehemu za siri maeneo ya makalioni kwa mjukuu wake mwenye umri wa miaka 7 mwanafunzi wa darasa la pili na Ayubu Mng’osi” ameeleza

Kamanda huyo alisema mtuhumiwa amekamatwa na upelelezi bado unaendelea .

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *