DESCHAMPS: Hakuna mbadala wa Benzema

Didier Deschamps

KOCHA wa Timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps hatomuita mshambuliaji yoyote kuchukua nafasi ya Karim Benzema aliyeumia mazoezini jana wakati timu hiyo ikijiandaa na mchezo wa kwanza wa Kombe la Dunia dhidi ya Australia November 22, 2022.

Benzema (34) atakosa mashindano ya Kombe la Dunia yanayoanza leo nchini Qatar kutokana na jeraha la paja alilopata mazoezini. Uchunguzi wa kitabibu umethibitisha kuwa mshindi huyo wa Ballon d’Or mwaka 2022 anahitaji wiki tatu kupona.


Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari mapema hii leo, alipoulizwa kama ataita mchezaji mwengine Deschamps alijibu “Hapana hakuna haja.” wakati huo tayari zilianza tetesi za kuitwa kwa mshambuliaji wa Manchester United Anthony Martial.

“Haifurahishi kamwe, haikufanyi utabasamu, tumempoteza Christopher Nkunku na kila mtu alihuzunika sana, jana ni Karim tuna malengo na tufahamu kundi linatusubiri.”amesema Deschamps

Taarifa njema zilikuwa ni juu ya urejeo wa beki wa Manchester United, Rafael Varane ambaye aliumia katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea. “Kila kitu kipo sawa, atakuwa fiti katika mechi ya kwanza dhidi ya Australia.

” ameongeza Deschamps.

Advertisement

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *