Dhoruba yaua 28 Marekani

WATU 28 wamekufa magharibi mwa Jimbo la New York, wengi wao kutoka Buffalo, wakati wa dhoruba kubwa ya msimu wa baridi ikiendelea kulikumba Taifa la Marekani.

Rais wa Marekani, Joe Biden ameidhinisha kupelekwa kwa msaada wa dharura katika jimbo hilo kufuatia janga hilo lililosababisha baadhi ya maelfu ya watu kuachwa bila nishati ya umeme.

Kikosi cha dharura cha uokoaji, kimeokoa walioathiriwa kutokana na kile mamlaka nchini humo imekiita dhoruba ya theluji ya karne na kutatiza mwenendo wa usafiri katika majimbo tisa.

Mamlaka katika jimbo la New York imeeleza hali kuwa mbaya zaidi hasa katika eneo la Buffalo huku miili ikigunduliwa kwenye magari, kingo za theluji na waokoaji wamekuwa wakikagua gari kwa gari wakitafuta waliofariki.

Gavana wa New York Katheleen Hochul, amesema wanatazamia dhoruba itarejea tena ambapo barafu yenye urefu wa inchi 6 hadi 12 upande wa kusini wa Kaunti ya Erie na kusini kidogo mwa eneo hilo walipata theluji yenye urefu wa inchi 30 hadi 40 usiku wa kuamkia leo, hivyo ni mapema kutabiri kama ndio mwisho.

Habari Zifananazo

Back to top button