Diamond aachia kitu kipya

MSANII wa muziki wa bongo fleva, Nassib Abdul ‘ Diamond Platnumz’, ametimiza ahadi yake kwa mashabiki wa muziki baada ya kuachia wimbo mpya mapema leo Julai 4, 2023.

Siku za hivi karibuni msanii huyo alichapisha kwenye ukurasa wake wa Intagram kuanzia Julai mwaka huu atakuwa akiachia ngoma kali bila kituo hadi mwakani.

Advertisement

Msanii huyo ambaye ni mmliki wa lebo ya muziki ya Wasafi, amesema  kwakuwa mwezi Julai ni mwezi wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mama yake, basi atakuwa akitesa katika soko la muziki hadi mwakani ambapo atampisha msanii mpya anayetarajiwa kutambulishwa kwenye lebo hiyo.

Diamond leo ameachia video ya wimbo mpya ujulikanao kama My Baby, aliomshirikisha msanii kutoka Nigeria, Chike Ezekpeazu Osebuka ‘Chike’.

1 comments

Comments are closed.