Diamond asaini mkataba kampuni ya mavazi
Kampuni ya mavazi ya vitenge, Hollantex itashirikiana na msanii wa kizazi kipya, Diamond Platnumz katika kampeni mpya ya kukuza matumizi ya mavazi ya vitambaa vya vitenge.
Kampeni hiyo Inayojulikana kama #togetherwithhollantex, itaenda sambamba na kutoa fursa kwa washiriki kutuma picha kwenye mitandao ya kijamii wakiwa na mavazi ya vitenda ambapo wataweza kushinda zawadi hadi Sh milioni 12.
“Kampuni yetu inaamini kuwa mavazi ya mitindo ya kiafrika ni njia moja wapo ya kutanabaisha utamaduni, kujieleza na kuunganisha na wengine,” ilisema taarifa ya Hollntex.
Kampeni hiyo inalenga pia kuibua na kuchochea umoja, kati ya watu wa rika na asili zote watakaoletwa pamoja kusherehekea utamaduni na urithi wao kwa pamoja.
Kwa mfano, hivi majuzi kundi la marafiki mjini Dar es Salaam walifanya kikao cha picha wakiwa wamevalia vitambaa vya Hollantex. Kikao hicho cha picha kilikuwa njia ya marafiki hao kusherehekea urafiki wao na upendo wao kwa utamaduni wa Afrika.
Picha hizo zilishirikishwa kwenye mitandao ya kijamii kwa hashtag #togetherwithhollantex, na zilivuma sana.
Kampeni ya #togetherwithhollantex ni mfano mzuri wa jinsi mitindo inaweza kutumika kukuza mabadiliko chanya ya kijamii.
Kampeni hiyo inasaidia kuondoa mipaka na kuleta watu pamoja, na ni ushuhuda wa nguvu ya mavazi na mitindo mbalimbali inavyoweza kutumika kuleta umoja kwa wanajamii