Diamond ataka wasanii kubadilika

Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewataka wasanii wa hapa nchini kujitangaza ili kutengeneza pesa na kuacha kuwekeza nguvu kubwa kwenye chati za muziki, ambazo hazilipi vizuri badala yake waangalie kwenye maslahi.

Akizungumza katika jukwaa la Acces alisema kuwa hivi sasa muziki umebadilika unahitaji uwekezaji mkubwa wa muda na fedha ili kutengeneza faida kubwa ambayo itamuongezea pato msanii ili aweze kufanya kazi nzuri na bora.

“Wasanii wanawekeza nguvu kubwa kwenye mtandao wa Youtube, lakini nao haulipi sana wanatakiwa kuanza kujiongeza kwa kufanya jitihada za kujitangaza zaidi kwenye mitandao tofauti tofauti, ambayo inalipa,”.

Advertisement

“Mfano You Tube, ukifikisha watazamaji milioni moja unapata kama kiasi hicho hicho cha pesa lakini mtandao kama Spotfy, unapata stream milioni moja unapata kama dola 3,000 karibu milioni saba hivi,” alisema iamond.

Alisema wasanii wa hapa nyumbani wanapaswa kubadilika kama walivyofanya wasanii wa mataifa mengine walishapiga hatua kwenye mitandao kama hiyo hivyo ni wakati wa wazawa kufanya jitihada hizo.