Diamond; Nikikupa moyo wangu unadondoka puuh!

DAR ES SALAAM: Staa wa Muziki wa Bongo Fleva Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz amesema yeye ni binadamu mvumilivu mno tofauti na watu wanavyomfikiria.

Diamond amesema watu wengi wanahukumu maisha yake bila kujua uhalisia akisema maisha yake ya mtandaoni ni ya tofauti na maisha halisi na wale wanaomfahamu wanalifahamu hilo.

Akizungumza leo Aprili 11, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akitambulisha Tamasha la Muziki litakalofanyika Aprili 26, 27 Viwanja vya Posta Dar es Salaam msanii huyo amesema sio rahisi kwa wengine kuyastahimili anayopitia.

“Kuna watu walikuwa wanasema tatizo Diamond akisemwa au akikosolewa anakasirika, Sheikh… mimi ndio mtu ninaeongelewa kwa maneno tofauti tofauti kuliko yeyote katika hili taifa, ushawahi kuniona nimejibizana hata siiku moja, moyo wangu nikikupa mimi unaweza kudondoka…nikikupa sasahivi ..ukifika hapo nje unadondoka Puuh!

“Miongoni mwa wasanii ambao ni komavu ,shupavu ni mimi , wewe andika sema chochote unachokitaka, sikujibu, sitetereki sanasana nikiona umezidi sana nitakutumia tuu barua, eeh bhana usinizungumzie imetosha , sikupeleki polisi wala sikudai hela” amesema msanii huyo.

Diamond amesema wasanii mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi watatumbuiza katika tamasha hilo la siku mbili.

Habari Zifananazo

Back to top button