Diamond Platnumz kivutio SBL ikija kivingine

Dar es Salaam: Serengeti imezindua upya muonekano mpya na aina mpya, Serengeti Lemon katika tukio la lililoandaliwa na Diamond Platnumz na kuhudhuriwa na watu mashuhuri wa Tanzania.

Muonekano huo mpya wa bia ya Serengeti yenye ladha ya limao ilionekana kuwakosha wageni hao kwa ladha na muonekano wake kwenye shughuli hio iliyofanyika Link Dar Lounge, Masaki usiku wa kuamkia leo.

Tukio hilo lililenga kuleta ari mpya na kuendelea kutimiza ahadi ya Serengeti ya kusherehekea umoja wa Tanzania. Muonekano mpya, wa kisasa, na wenye nguvu unawakilisha safari ya bia ya Serengeti na dhamira yake ya maendeleo ya muda mrefu pamoja na bidhaa za ubunifu kama Serengeti Lager, Serengeti Lite, na sasa Serengeti Lemon.

“Kama chapa ya bia inayoongoza nchini Tanzania, tunafurahia safari hii mpya inayowakilisha roho ya ustahimilivu na kujitolea kwa Watanzania. Serengeti ni chapa changa iliyoanzishwa mwaka 1996, na kwa sababu ya upendo na fahari ya Watanzania, chapa hii imekua kuwa chapa kubwa zaidi ya bia iliyofungwa chupa katika Afrika Mashariki,” alisema Obinna Anyalebechi, Mkurugenzi Mkuu wa SBL.

‘Tunafurahi sana kwakuwa chapa yetu ya Serengeti inaendelea kuwakilisha nguvu na upekee wa nchi yetu,Tanzania, na muonekano huu mpya unadhihirisha dhamira yetu ya kusonga mbele tukiwa pamoja na watu wetu’. Alisema Anitha Rwehumbiza, Mkurugenzi wa masoko SBL.

 

Habari Zifananazo

Back to top button