Diamond: Siongei sana, nishavuka huko

DAR ES SALAAM :Msanii wa Bongo Fleva Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz amesema mwaka huu amejipanga kufanya muziki mzuri wa ndani na kimataifa.
Akizungumza leo wakati alipozindua tamasha la muziki litakalofanyika Aprili 26, 27 Viwanja vya Posta Jijini Dar es salaam msanii huyo amesema hana muda wa maneno bali kazi zake zitaongea.

 
” Inshallah kwangu mimi nitazameni tuu mimi ni mbishi sana na mwaka huu ni hesabieni viwanja vyangu navyovifanya nihesabieni ‘Arena’ zangu nazozifanya mimi siongei sana nishavuka kuongea..
“Mimi nafanya matukio makubwa mwaka huu tunadondosha ngoma nzito, ngoma za ndani na nje .

“Amesema Diamond.

Tamasha hilo litashirikisha wasanii kutoka ndani nje ya nchi huku akiwaomba wasanii kushiriki kwani lengo lao ni moja kuukuza muziki wa Tanzania.

Habari Zifananazo

Back to top button