Mwimbaji na Muigizaji mkongwe nchini Marekani Diana Ross, leo anasheherekea siku yake ya kuzaliwa. Alizaliwa Machi 26 , 1944 huko Detroit Michigan nchini Marekani.
Diana Ross alianza safari yake ya uimbaji na uigizaji wakati akiongoza kundi la The Supremes, na kundi hili liliweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika miaka ya sitini na kumuwezesha Diana Ross kuuza nyimbo nyingi ndani ya Marekani na nje ya Marekani .
Na mpaka sasa kundi hili the The Supremes bado linaendelea kuacha historia nchini Marekani kwa kazi zake za muziki na limebaki kundi bora lenye chati bora katika Billboard Hot 100 ya Marekani.
Miongoni mwa nyimbo bado zinakiki ni Where Did Our Love Go, Baby Love, Come See About Me bila ya kusahau Love Child.
Mwaka 1970, Diana Ross alijiondoa katika kundi hilo la Supremes na kuamua kusimama mwenyewe katika kazi za muziki wa solo. Kazi hizi zilimuwezesha kutoa albamu yake ya kwanza iliyokuwa na nyimbo zake tu.. inayojulikana kama Ain’t No Mountain High Enough.
Mwaka huohuo alifanikiwa kutoa albamu nyingine Everything Is Everything. Albamu hii ilimuwezesha Diana Ross kumuweka katika nafasi bora zaidi kwa vibao vyake alivyoweza kuvitoa ikiwemo I’m Still Waiting.
Diana Ross aliendelea kufanya kazi yake kwa ueledi mkubwa na hatimaye jina lake kuwekwa katika rekodi bora duniani za muziki kwa kufanya matamasha na ziara mbalimbali za muziki.
Ushiriki wake huo wa matamasha na kufanya ziara mbalimbali za muziki umemsaidia Diana Ross kuwa na nafasi nzuri ya kuzungumziwa katika televisheni mbalimbali nchini Marekani, ambapo ulimsaidia Diana Ross kutoa vibao vingi vya muziki.
Albamu zake zilizokiki katika mwaka wa 1973 ni Touch Me In the Morning, Mahogany aliyoitoa mwaka 1975, nyingine Diana Ross iliyotikisa mwaka 1976 na Diana mwaka 1980.
Vibao vilivyokiki zaidi na kupendwa ni Touch Me In The Morning, Theme From Mahogany, Do You Know Where You’re Going To, Love Hangover na Endless Love.
Mafanikio mengine ya kibiashara aliyoweza kupata Diana Ross katika miaka ya 1980 na 90 ni kutoa vibao vingine vya kimataifa vikiwemo I’m Coming Out, Why Do Fools Fall in Love na Chain Reaction.
Katika tasnia ya uigizaji , Diana Ross alikuwa na ndoto ya kupata tuzo ya Golden Globe kwa uigizaji wake. Aliteuliwa na Billie Holiday katika filamu ya Lady Sings the Blues mnamo mwaka 1972
Kufuatia kazi zake za sanaa ya uigizaji na uimbaji Diana Ross alikuwa mwigizaji wa kwanza Mwafrika kutoka Marekani kupokea Tuzo ya Academy.
Katika masuala ya uigizaji wa filamu Diana Ross pia alifanikiwa kurekodi sauti yake na kutengeneza albamu yake ya kipekee ambayo ilitambulika albamu ya kwanza iliyokuwa katika chati za Billboard 200.
Aliigiza pia katika filamu zingine mbili, Mahogany mwaka 1975 na The Wiz mwaka 1978 na baadaye alionekana katika filamu za televisheni Out of Darkness mnamo mwaka 1994, ambazo zilimfanya kuteuliwa kupata tuzo ya Golden Globe, na Double Platinum mwaka 1999.
Kwa kazi zake hizi za sanaa ya uigizaji na uimbaji Diana Ross akabatizwa jina lingine ambalo lilivuma katika mwaka 1976 na kuitwa: “Female Entertainer of the Century” .
Tangu alipoanza kusimama akiwa mwenyewe Diana Ross ameshatoa albamu zisizopungua 25 za studio zenye nyimbo nyingi na kufanikiwa kuuza rekodi milioni 100 duniani kote.
Yeye ndiye msanii wa pekee mwanamke kuwa na nyimbo za kwanza kwenye Billboard Hot 100 mwaka 2021, Billboard ilimweka Diana Ross miongoni mwa wasanii 30 bora wa Hot 100 na aliyekaa kwenye chati za Billboard Hot 100 kuanzia mwaka 1955 hadi 2018 mfululizo.
Mnamo mwaka 1988, Diana Ross aliingizwa kwenye Rock and Roll Hall of Fame kama mshiriki wa kundi la Supremes, na ni mmoja wa wasanii adimu ambao wana nyota mbili kwenye Hollywood Walk of Fame.
Kazi yake hii ilimuwezesha Diana Ross kupokea tuzo mbalimbali, alishawahi kupokea tuzo maalum ya Tony mnamo mwaka 1977, alipokea tuzo nyingine ya heshima ya Kennedy mwaka 2007, Tuzo ya Mafanikio ya Maisha ya Grammy mwaka 2012 na 2023 na tuzo hii ilimfanya Diana Ross kuwa mwanamke wa kwanza kushinda mara mbili na alipatiwa nishani ya Rais ya Uhuru mwaka 2016.
Leo Diana Ross anatimiza miaka 80 tangu kuzaliwa kwake ..Dailynews Digital inamtakia kila la heri. Happy Birthday Diana Ross ….