KOCHA msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze amethibitisha kuwa kipa wao Djigui Diarra atakosekana kwenye mchezo wa kesho wa Ligi Kuu dhidi ya Singida Big Stars utakaopigwa saa 1:00 usiku Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Kaze amesema mchezaji huyo pamoja na wengine Gael Bigirimana na Aziz Ki ambaye alifungiwa michezo mitatu na Bodi ya Ligi wameruhusiwa kwenda kujiunga na timu zao za taifa.
Kaze amesema mchezo huo utakuwa mgumu kwa Yanga hasa kutokana na ubora wa wapinzani wao na kuwa na kocha mwenye uzoefu.
…Mechi yetu na Singida big Stars ni mchezo mgumu kutokana na ukubwa wa kikosi cha Singida hasa ukizingatia mwalimu waliye nae (Hans) ni mzoefu sana na amewahi kuitumikia Yanga SC kwa mafanikio…
…Kuwa unbeaten haitupi sisi presha yoyote, sisi tunacheza kwa malengo yetu ya kupata mataji hivyo kila mechi tunahitaji kujiandaa na kushinda. Unaweza kuwa unbeaten na usiwe bingwa hivyo haitakuwa na maana. Hatujiwekei presha kubwa ya unbeaten tunacheza kwa malengo.” amesema Kaze