Dier kutua Bayern leo

KIUNGO wa raia wa Uingereza, Eric Dier leo atajiunga na Bayern Munchen kwa dau la pauni milioni 4 akitokea Tottenham Hotspurs.

Taarifa ya mwandishi wa habari za michezo kutoka nchini Italia, Fabrizio Romano imeeleza kuwa Dier 29, mwenye uwezo wa kucheza beki wa kati, ameshawasili jiji la Munich na atakamilisha vipimo vya afya leo.

Spurs wanamuachia Dier baada ya kuwa na uhakika wa kumsajili Radu Dragusin kutoka Genoa ambaye tayari amekamilisha vipimo vya afya jana.

“Eric Dier yuko hapa jijini na tunajaribu kukamilisha uhamisho wa kumpata kama chaguo jingine kama beki wa kati tutasubiri hadi kila kitu kimamilike.” Amesema kocha wa Bayern Thomas Tuchel.

Habari Zifananazo

Back to top button