DIT kutengeneza vipuri vya vyombo moto, mitambo

TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imeanza kutengeneza vipuri vya magari, pikipiki na bajaji.

Mtaalamu wa vipuri kutoka DIT, Abdul Rwangisa akizungumza na HabariLeo leo Juni 30, 2023 katika maonyesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ‘Sabasaba’ amesema DIT mbali na vipuri hivyopia kuna wanatengeneza vipuri vya mitambo mbali mbali

Amesema, DIT imejikita katika kutengeneza vipuri mbali mbali ili kuondoa changamoto iliyopo mitaani.

“Tumekuja na suluhisho kwa kuwaletea spea wananchi kwa gharama nafuu na zimetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu, tumeangalia hali na uhitaji uliopo mitaani.”Amesema Rwangisa na kuongeza

“Spea za magari tulizonazo ni za  Hiace, Heiche, Hilux na Subaru, na kama mtu anachangamoto ya spea katika gari lake atuletee sisi tutaipima, tutatengeneza.”Amesema

Amesema, tayari vipuri hivyo vya vyombo vya moto vimeshasambazwa na kuanza kutumika katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Mbeya na Songwe.

“Tulishapeleka TBS kwa ajili ya kucheki ubora na kupata cheti chetu, ushauri kwa watanzania tutumie bidhaa za nyumbani hata ikitokea kuna tatizo ni rahisi kwenda kwa mtengenezaji na kuwasilisha tatizo lako kama bidhaa yako ipo hivi vile lazima zitaboreshwa, vya nje zikiwa na tatizo uwezi kupata suluhisho.”Amesema

Aidha, amesema maoni ambayo wamepata kwa watumiaji hususani wa bajaji ni kwamba bidhaa za kutoka nchi nyingine wananunua kila wiki vipuri lakini tangu wameanza kutumia bidhaa zetu wananunua baada ya mwezi.

Amesema, kwa sasa wanatengeneza ‘package’ ya moja kwa moja ambayo inaenda kwa mtumiaji.

Habari Zifananazo

Back to top button