DIT wajipanga kurusha satelaiti mwaka 2024
DAR ES SALAAM; TAASISI ya Teknolojia Dares Salaam (DIT), imesema kufikia 2024 wataweza kurusha satelaiti nchini, ikiwa ni hatua inayotokana na kuongezeka kwa ujuzi, ubunifu na teknolojia.
Mkuu wa Taasisi hiyo, Profesa Preksedis Ndomba amesema hayo leo Dar es Salaam kwenye mahafali ya 17 duru ya kwanza ya DIT, ambapo jumla ya wanafunzi 1225 wa ngazi mbalimbali za masomo wamehitimu.
Kuhusu satelaiti amesema tayari chuo hicho kimeingia mkataba na chuo kikuu cha RUDN cha Urusi na hatua hiyo imefikiwa kutokana na kubadilishana uzoefu kati ya taasisi hiyo na wataalamu wengine kutoka ndani na nje ya nchi.
Pia amesema mbali ya chuo hicho, taasisi pia inashirikiana na Marekani katika eneo la TEHAMA, Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP) kwenye kukuza matumizi bora ya nishati na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kwenye eneo la tiba mtandao.
Amesema ushirikiano huo umekuwa na manufaa kwa taasisi hiyo kwa kuwa watumishi wake wanaongeza ujuzi unawafikia vyema wanafunzi katika nyanja mbaimbali za masomo.
Kuhusu mahafali amesema jumla ya wahitimu 1225, wanaume wakiwa 923 na wanawake 302, wametunukiwa tuzo mbalimbal