TAASISI ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) imezindua teknolojia ya tiba mwanga ‘Phototherapy’ kwa ajili ya Watoto njiti wenye matatizo ya homa ya manjano.
Mashine hiyo ya tiba mwaga aina A, imeshapelekwa katika hospitali za Muhimbili Upanga, Mloganzila, Amana na Kigamboni.
Teknolojia hiyo imebuniwa na mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa chuo hicho Joshua Macha.
Akizungumza na HabariLeo katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara, Joshua amesema kuwa kifaa hicho kinasaidia kutibu watoto wachanga hususani watoto njiti wenye matatizo ya manjano ya ngozi
“Watoto njiti wanapozaliwa miili yao inashindwa kumengenya protein hadi kufikia hatua ya mwisho, kwa hiyo ile protein inatoka inakuja kukaa kwenye ngozi na kupelekea kuziba mishipa ya damu, mwisho wa siku damu ikishindwa kutembea mtoto anapoteza maisha.”Amesema Joshua na kuongeza
“Hivyo tumekuja na hiki kifaa ili kuondoa hilo tatizo, tumetumia mionzi taipu A, mionzi hii mtoto atakuwa anawekwa kwenye hiki kifaa na kumulikwa na hiyo mionzi juu na nchi ili iweze kumpiga mwili mzima.
“Mionzi hii inapommulika, inasaidia kuyeyusha protein iliyopo kwenye ngozi na mkusaidia kumuepusha na kifo kitokanacho na manjano, na mtoto atawekwa kwa muda ambao daktari ataona inafaa kutokana na hali ya ugonjwa wa mtoto.
Amesema, mionzi taipu A haina athari zozote kwa mwili wa mtoto, shida tu inakuja kwenye macho, mtoto mchanga bado macho hayajakomaa kwa kuwa mwanga ni mkali unaweza kumpofua macho ndio maana anafunikwa macho ila katika mwili hakuna madhara yoyote.
Tumekuja na hiki kifaa baada ya kufanya tafiti katika hospitali mbali mbali ikiwemo Amana, Mloganzila na Kigamboni tuligundua Watoto wanaokumbwa na changamoto wapo wengi lakini vifaa ni vichache, kwa sababu vinaagizwa nje ya nchi na gharama yake ni kubwa na vile vile ikitokea umepata hitilafu yoyote matengenezo yake pia ni shida.
Tumekuja na kifaa hiki ili kuokoa maisha ya Watoto kwa gharama rais, hospitali yoyote inaweza kuzinunua, na ikitokea imeleta hitilafu marekebisho ni rahisi kwa sababu vimetengenezwa kwa material za hapa hapa nyumbani hivyo kurekebisha inakuwa ni rahisi.
Mashine ya nje gharma milioni 6 mashine yetu ni milioni 2.5.
Kwa sasa tupo kwenye hatua ya ukaguzi na kupata kibali ili tuanze kutengenza na kuziuza katika mahospitali mengine.
Comments are closed.