Ditopile akoleza kauli ya Rais Samia

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile ameunga mkono kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa siku juzi siku ya mashujaa kuwa Tanzania ni moja na haigawanyiki.

Ditopile ametoa kauli hiyo, katika mkutano wa hadhara wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Abdulrahman Kinana uliofanyika katika uwanja wa Mkendo, Musoma mkoani Mara.

“Lakini kwa vile nimetoka Dodoma na nimefika hapa, wakati nakuja nilisimama Bunda kupata kahawa kidogo pembeni nimeona kaduka kadogo dogo kameandikwa dawa za kisuna, nikasogea kujua dawa za kisuna ni zipi nimekuta kuna hudi.

Advertisement

” Lakini pia nimekuta sehemu kuna Mpemba anauza changu, changu ndani ya Mara, changu oyeee, kuna siku nilikua Zanzibar nilimkuta Chacha, Chacha oyee.

“Lengo la kusema hivyo ni kuunga,kukoleza kauli ya Rais wakati anaadhimisha mashujaa, Tanzania ni moja na haigawanyiki. ” Amesema

Aidha, Ditopile amemwagia sifa Kinana na kudai kuwa hata kama hapendi kusifiwa lakini ni lazima watamsifu wakati yupo hai ili asikie kwa masikio yake.

“Makamu Mwenyekiti najua hupendi kusifiwa, lakini kwa kazi kubwa uliyoifanyia chama hiki na nchi hii hatuwezi kunyamaza kukusifia wakati tunambiwa msifie mtu wakati bado yupo hai na usikie kwa masikio yako.

“Ulichaguliwa kuwa mlezi wa Mara, umetembea nchi hii kupigania Chama, wana Mara wana matumaini makubwa sana, hadhara hii ya Mara ipo tayari kukusikiliza

“Niseme Kamati Kuu imetumia vigezo na masharti , uzuri jana ulipita kwa Mkuu wa Majeshi Mstaafu upate baraka zake kwa sababu sifa kubwa ya Mkoa huu ndio watu waliojaza Jeshi letu, kama tunavyojua wewe ni Kanali Mstaafu tena sio Kanali hewa, umeshiriki kwenye vita ya kumfukuza Nduli Idd Amini.

“Kwa hiyo kwa sifa hiyo, Wana Mara mmepata mlezi madhubuti, na hao wanaopiga kelele kazi wanayo, moto wa Kinana wautaweza??” Amesema kwa kuhoji na kuitikiwa na umati wa watu kuwa hawawezi.