MBUNGE viti Maalum Mkoa wa Dodoma anayetokana na Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Mariam Ditopile amewawezesha wanafunzi wenye mahitaji maalumu vifaa vya shule kwa wanafuzi 1000 vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 30.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo kwa wilaya zote saba za Dodoma, Ditopile amesema ni kusherehekea kumbukizi ya kuzaliwa Rais Samia Suluhu Hassan aliyeadhimisha siku hiyo jana Januari 27,2023.
Aidha, amewaomba wadau mbalimbali mkoani humo na kutoa kipaumbele zaidi katika sekta ya elimu kwa kutoa misaada hasa wa watoto yatima na wenye mazingira magumu.