Diwani, wengine 19 mbaroni kwa viuatilifu Masasi

Diwani, wengine 19 mbaroni kwa viuatilifu Masasi

WATU 20 akiwemo diwani wa Kata ya Lulindi Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, mkoani Mtwara wamekamatwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa kwa kukutwa na viuatilifu mbalimbali vyenye ruzuku ya serikali kinyume cha sheria.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Isack Mishi amewaambia waandishi wa Habari leo kuwa watuhumiwa hao walikamatwa wilayani Masasi katika oparesheni ambayo ilifanywa na polisi Agosti 16, mwaka huu.

“Kufuatia taarifa fiche za kuwepo kwa viuatilifu hivyo bila utaratibu, ndipo polisi kwa kushirikiana na mamlaka za Bodi ya Korosho Tanzania (CBT)  na mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA) zilianza oparesheni ya pamoja na kuwakamata watuhumiwa 20,” amesema.

Advertisement

Amesema uchunguzi wa awali umebainisha kuwa wapo pia wafanyabiashara wanaorubuni wakulima kuwauzia viuatilifu hivyo, kwa bei ya chini kisha wao kwenda kuviuza kwa bei ya juu zaidi katika maduka yao.

/* */