Djokovic akemea vurugu Serbia

MKALI wa Tennis kutoka Taifa la Serbia, Novak Djokovic amechukizwa na kukemea vurugu zinazoendelea nchini humo kwa kusema “Kosovo ni moyo wa Serbia. Acha vurugu”.

Ujumbe huo ameutoa jana baada ya mapigano kuzuka Kaskazini mwa Kosovo kubwa ikiwa ni mivutano ya kikabila.

Djokovic mzaliwa wa Belgrade aliandika ujumbe huo kwa Kiserbia baada ya ushindi wake wa raundi ya kwanza dhidi ya Aleksandar Kovacevic kwenye onesho la Philippe Chatrier Court huko Roland Garros.

“Kosovo ndio chimbuko letu, ngome yetu, kitovu cha mambo muhimu zaidi kwa nchi yetu… Kuna sababu nyingi kwa nini niliandika hivyo,” Djokovic mwenye umri wa miaka 36 aliambia vyombo vya habari kwenye michuano hiyo.

Walinda amani wanaoongozwa na NATO jana waliwatawanya waandamanaji Waserbia ambao walikabiliana tena na polisi Kaskazini mwa Kosovo kutaka mameya waliochaguliwa hivi karibuni wa Albania kuondolewa madarakani, huku mizozo ya kikabila ikipamba moto katika taifa hilo la Balkan.

Takriban wanajeshi 25 walijeruhiwa wakati wa mapigano hayo, pamoja na zaidi ya waandamanaji 50.
Waserbia wa Kosovo walikuwa wamesusia uchaguzi wa mwezi uliopita katika miji ya kaskazini, ambayo iliruhusu Waalbania wa kabila kuchukua udhibiti wa mabaraza ya mitaa licha ya kujitokeza kwa idadi ndogo ya chini ya asilimia 3.5 ya wapiga kura.

Serikali ya Waziri Mkuu wa Kosovo, Albin Kurti, iliwaweka rasmi mameya hao wiki iliyopita, na kukaidi wito wa kupunguza mivutano ya Umoja wa Ulaya na Marekani, ambazo zimepigania uhuru wa eneo hilo kutoka kwa Serbia mwaka 2008.

Habari Zifananazo

Back to top button