Dk Biteko: Wazanzibari ni wakarimu sana

Awaasa Watanzania kuwaombea viongozi wao

UNGUJA, Zanzibar: NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk Doto Biteko amesema tangu amefika visiwani Zanzibar, amevutiwa na ukarimu, tenzi na ufundi wa kuimba kutoka kwa watu wa Zanzibar.

Dk Biteko amesema hayo leo, Wilaya ya Magharibi A, Mkoa wa Mjini Magharibi katika hafla ya utiaji saini mkataba wa mauziano ya gesi asilia kati ya Serikali na wawekezaji.

“Moja ya utenzi ulionifurahisha sana ni mpewa hapokenyeki, aliyepewa kapewa hata ukinuna,” amesema Dk Biteko

Amekiri kufurahishwa na kasi ya utendaji kazi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kutengeleza miradi mingi ya maendeleo yenye tija kwa taifa.

“Dk Hussein Ali Mwinyi anafanya kazi nzuri sana. Jamani, hapa unazindua miradi mpaka unachoka. Unaona mambo anayofanya mama (Rais Samia Suluhu Hassan) kule bara, hapa pia kasi ile ile.

” Amesema kiongozi huyo.

Kwa upande mwingine, amewataka Watanzania kuona haja ya kuungana pamoja kuwaombea viongozi wa Taifa, katika kipindi hiki kuelekea kilele cha Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar.

Habari Zifananazo

Back to top button