Dk Kiruswa azindua mfumo ushirikishwaji jamii

Dk Kiruswa azindua mfumo ushirikishwaji jamii

NAIBU Waziri wa Madini, Dk Steven Kiruswa amezindua  mfumo wa ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya madini na wa utoaji wa huduma kwenye jamii unaofanywa na migodi ya madini.

Dk Kiruswa amefanya uzinduzi huo katika Jukwaa la Pili la Utekelezaji wa Ushirikishwaji wa Watanzania katika Sekta ya Madini linaloendelea jijini Arusha, linalokutanisha  kampuni za uchimbaji  wa madini, watoa huduma wa madini kwenye migodi ya madini na taasisi za kifedha.

Akizungumzia  mfumo huo, Naibu Waziri  Kiruswa amesema utawezesha kampuni za uchimbaji wa madini na watoa huduma kwenye migodi ya madini kuwasilisha nyaraka mbalimbali kuhusu ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya madini na utoaji wa huduma kwa jamii kwenye migodi ya madini kwa njia ya kieletroniki, badala ya kutumia nakala ngumu kama ilivyokuwa awali.

Advertisement

Amesema mfumo pia utarahisisha kazi ya uchakataji wa maombi yanayowasilishwa Tume ya Madini na majibu  ya maombi kutolewa kwa wakati na watalaam kutoka Tume ya Madini.

Add a comment

Toa Jibu

Barua-pepe haitachapishwa. Fildi za lazima zimetiwa alama ya *