Dk Kiruswa kufunga Jukwaa la Madini

ARUSHA; NAIBU Waziri wa Madini, Dk Steven Kiruswa ametembelea maonesho, ikiwa ni sehemu ya Jukwaa la Tatu la Ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya madini linalohitimishwa leo Mei 24, jijini Arusha.

Dk Kiruswa anatarajiwa kufunga jukwaa hilo sambamba na kutoa tuzo na vyeti mbalimbali kwa wadhamini.

Jukwaa hilo lilianza mapema Mei 22, 2024 likikutanisha wadau  mbalimbali ikiwa ni pamoja na wamiliki wa leseni za madini, watoa huduma kwa wamiliki wa leseni za madini, Taasisi za Fedha na Taasisi za Serikali.

Habari Zifananazo

Back to top button