Dk Lucy achomoza mshindi utumishi wa umma

DAR ES SALAAM; Dk Lucy Shule ambaye ni Mkurugenzi wa Mafunzo katika Chuo cha Ulinzi cha Taifa (NDC), ameibuka kinara kwenye Tuzo ya Uongozi katika sekta ya utumishi wa umma katika Tuzo za Malkia wa Nguvu 2024 zilizofanyika usiku wa Machi 23, 2024 ukumbi wa Mlimani City.

Dk Lucy kwa zaidi ya miongo miwili amehudumu kwenye masuala ya ulinzi na usalama na amefanya tafiti nyingi kuhusu masula ya ulinzi na usalama, utatuzi wa migogoro, diplomasia na uhusiano wa kimataifa.

Advertisement

/* */