Dk Mollel ataka kampeni kusambaza taulo za kike mashuleni

ARUSHA: NAIBU Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel amewataka wadau wa afya zikiwemo taasisi za Umma, Asasi na Mashirika yasiyo ya Kiserikali NGO’S kuhakikisha wanaanzisha kampeni za kusambaza taulo za kike bure mashuleni ili ziweze kumsaidia mtoto wa kike pindi anapoingia katika siku zake akiwa shuleni.

Mollel amesema hayo leo katika kilele cha Siku ya Hedhi Salama Duniani ambapo Kitaifa ilifanyika jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali na chama na serikali na wadau mbalimbali wa sekta ya afya na kusema kuwa kampeni hiyo inaweza kumsaidia sana mtoto wa kike akiwa shuleni.

SOMA: Wanafunzi wa kike wapewa msaada wa taulo

Amesema pamoja na mipango mizuri ambayo imefanywa na Jukwaa la Hedhi Salama Kitaifa pia ni wakati sasa jukwaa hilo pamoja na wadau wengine wa sekta hiyo kuhakikisha wanafanya kampeni ya kukusanya fedha kutoka kwa watu binafsi,taasisi za umma.

Waziri Mollel amesema TAMISEMI imeshajipanga kujenga vyumba maalumu kwa shule za msingi na sekondari kwa ajili ya mtoto wa kike pindi anapoingia katika siku zake aweze kubadilisha taulo ya kike na kuendelea na masomo hivyo basi taasisi,asasi na NG’O’S zinapaswa kujipanga kwa hilo ili kumwondolea mzigo wa mawazo mtoto wa kike.

Aidha Mollel ameitaka Wizara ya Afya kushirikiana na Hedhi Salama Kitaifa na wadau wengine wa sekta ya Afya kuhakikisha wanashirikiana katika kuelimisha jamii juu ya matumizi sahihi ya taulo ya kike kwa mtoto wa kike kwani huo sio ugonjwa kama inavyotasfriwa na baadhi ya jamii zisizo na uelewa wa jambo hilo.

Habari Zifananazo

Back to top button